• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Fainali ya Kombe la Ligi EPL

    (GMT+08:00) 2017-02-27 08:27:14

    Zlatan Ibrahimovic amepiga bao 2 wakati Manchester United wakiifunga Southamton 3-2 katika fainali ya kombe la ligi huko Uingereza, iliyochezwa uwanjani Wembley jijini London.

    Manchester walitangulia kwa bao 2-0 kwa mabao ya Ibrahimovic aliyefungwa kwa Freekick na Jesse Lingard, lakini mchezaji mpya wa Southampton aliwapa matumaini mashabiki wa timu hiyo kwa kufunga goli zuri kabla ya mapumziko. Hadi wakati wa mapumziko Man U walikuwa wakiongoza 2-1 dhidi ya Southampton.

    Dakika ya 48 ya kipindi cha pili, Southampton waliongeza bao kupitia kwa Manolo Gabbiadini, lakini zikiwa zimesalia dakika 3 kabla ya mchezo kumalizika, Man U walifanya Kaunta Attack, krosi safi ya Ander Herrera ilitua kichwani mwa Ibrahimovic aliyefunga goli la 3.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako