• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Wapiganaji 6 wa kundi la Taliban wauawa kaskazini mwa Afghanistan

    (GMT+08:00) 2017-02-27 16:40:38

    Wapiganaji sita wa kundi la Taliban wameuawa na wengine 12 kujeruhiwa ndani ya saa 24 zilizopita katika operesheni ya jeshi la nchi hiyo dhidi ya kundi hilo katik mkoa wa kaskazini wa Kunduz.

    Kati ya wapiganaji waliouawa ni makamanda wawili wa kundi hilo waliofahamika kwa majina ya Qari Aminullah na Hussain. Hata hivyo wapiganaji wa kundi hilo wanaodhibiti baadhi ya maeneo ya mkoa wa Kunduz hawajatoa tamko lolote kuhusiana na shambulizi hilo.

    Wakati huohuo, mkuu wa polisi mkoa wa Baghlan Noor Habib Gulbahari amesema, wapiganaji wanne wa kundi la Taliban wameuawa na vijiji kadhaa kukombolewa kutoka kwa kundi hilo katika mkoa huo.

    Jeshi la serikali ya Afghanistan lilifanya mashambulizi makali mwishoni mwa wiki iliyopita kuwaondoa wapiganaji wa kundi la Taliban katika maeneo yao kwenye wilaya za Dand-e-Ghori na Dan-e-Shahabudin mkoani Baghlan.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako