• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Polisi nchini Indonesia wamkamata mpiganaji baada ya shambulizi la bomu mkoa wa Java

    (GMT+08:00) 2017-02-27 16:40:56

    Polisi wa kitengo cha kupambana na ugaidi nchini Indonesia wamemkamata mtu anayetuhumiwa kuwa gaidi baada ya mtu huyo kulipua bomu na kuchoma jengo la ofisi katika mji mkuu wa mkoa wa Java Magharibi.

    Mkuu wa polisi wa mkoa huo Inspekta Jenerali Anton Charlian amesema, mtu huyo alilipua bomu moja kati ya mawili aliyokuwa nayo katika bustani ya Pandawa huko Bandug, mji mkuu wa mkoa wa Java Magharibi na kukimbilia kwenye ofisi ya kijiji cha jirani cha Pandawa na kuchoma jengo la ofisi hiyo.

    Inspekta Jenerali Charlian amesema, mtu huyo ni mwanachama wa kundi la kigaidi ambalo limetambuliwa kuwa mtandao wa siku nyingi wa kigaidi. Polisi pia wamekamata bunduki na mfuko baada ya kumkamata mtuhumiwa huyo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako