• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kenya: Marekani kupatia Kenya kibali cha usalama kwa ndege ya moja kwa moja

    (GMT+08:00) 2017-02-27 19:32:38

    uamuzi na mamlaka ya Marekani kupatia Kenya kibali cha usalama kwa ndege ya moja kwa moja kuenda marekani itapiga jeki mtiririko wa uwekezaji kutoka kwa nchi kubwa zaidi kiuchumi duniani, maafisa wa serikali wamesema.

    Idhini ya JKIA ilitokana na baada ya ukaguzi kufanyikiwa na kufikisha viwango vilivyowekwa na Shirika la Kimataifa la Usafiri wa Anga.

    Waziri wa Hazina ya fedha Henry Rotich amesema hatua hii itaongeza idadi ya watalii kutoka Marekani katika miaka ijayo.

    Siku za nyuma Kenya ilikuwa inatumia mashirika ya ndege mbalimbali kusafirisha bidhaa zao katika soko la Marekani lakini kuanza kwa ndege ya moja kwa moja mambo yatabadilika na sekta ya kilimo cha maua kitakuwa mlengwa muhimu.

    Thamani ya uagizaji wa bidhaa kutoka Marekani imeshuka kwa asilimia 187.20 na kufikia sh bilioni 43.89 mwaka jana kutoka Sh bilioni 126.05 bilioni katika mwaka wa 2015, Ofisi ya Taifa ya takwaimu ya Kenya imeonyesha.

    Mauzo ya nje, kwa upande mwingine, ilipanda hadi asilimia 7.57 hadi sh bilioni 43.47 kutoka sh bilioni 40.41.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako