• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China yasema Marekani na Korea Kusini zitawajibika na matokeo yanayowezekana kutokana na kuwekwa kwa THAAD

    (GMT+08:00) 2017-02-27 19:55:37

    China imepinga kuwekwa kwa mfumo wa kujilinda na makombora wa Marekani THAAD nchini Korea Kusini, ikisema itachukua hatua zinazohitajika kulinda maslahi yake ya usalama na kwamba Marekani na Korea Kusini zitatakiwa kuwajibika na matokeo yote yanayowezekana.

    Habari zinasema bodi ya wakurugenzi ya kampuni ya Lotte imekutana leo na kuidhinisha makubaliano ya kukabidhiana ardhi kati ya jeshi na Lotte, hatua inayolenga kuwekwa kwa THAAD.

    Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya China Geng Shuang amesema, uwekaji wa THAAD uliopendekezwa na Marekani na Korea Kusini umeharibu vikali uwiano wa kimkakati wa kikanda na maslahi ya usalama wa kimkakati wa nchi ikiwemo China, na pia hausaidii amani na utulivu wa Peninsula ya Korea.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako