• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kenya:Serikali yaitaka kampuni ya TAXI ya Uber kuboresha bei zao kwa ushindani sahihi

    (GMT+08:00) 2017-02-28 20:03:05

    Serikali ya Kenya imeitaka kampuni ya usafiri wa kibinafsi ya UBER kuboresha bei zao kwa ajili ya ushindani sahihi wa biashara nchini Kenya.

    Hii ni baada ya kampuni nyingine za kufanya kazi ya TAXI nchini Kenya kulalamikia kuhusu uharibifu wa kazi ulioletwa na Uber iliyopunguza kwa kiasi kikubwa bei .

    Madereva wa Taxi nchini wameandaa migomo ya mara kwa mara kupinga Uber wakidai imeshukisha bei pakubwa na kuharibu ushindani wa kibiashara.

    Katibu wa kudumu wa wizara ya uchukuzi Irungu Nyakera amesema wamekubliana kuhusu kiwango cha chini zaidi kwa kila mfanyibiashara hiyo ili hali ya biashara iregee kawaida kwa kila mmoja.

    Wateja wengi hata hivyo wameunga mkono na kuipenda kampuni hiyo wakielezea kwamba imerahisisha usafiri haswa wakati wa dharura na usiku ambapo Taxi aina nyingine huitisha pesa nyingi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako