• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Yanga yapoza machungu yake kwa kuipigisha kwata Ruvu Shooting

    (GMT+08:00) 2017-03-02 09:39:34

    Mabingwa watetezi wa ligi kuu Tanzania Bara, Yanga imefanikiwa kupoza machungu ya kufungwa na Simba mwishoni mwa wiki iliyopita baada ya jana kuwapigisha kwata maafande wa Ruvu Shooting kwa kipigo cha mabao 2-0. Mabao ya Yanga yalifungwa na Saimon Msuva dakika ya 31 kwa mkwaju wa penati uliopatikana baada ya beki wa Ruvu kuunawa mpira katika eneo la hatari, huku la pili likifungwa kwa ustadi mkubwa na Emmanuel Martin kwa kichwa akimalizia kros ya Saimon Msuva.

    Ushindi huo unaifanya Yanga ifikishe pointi 52 baada ya kucheza mechi 23, ikiendelea kukamata nafasi ya pili, nyuma ya vinara Simba SC wenye pointi mbili zaidi ingawa nao wamecheza mara 23.

    Yanga iliyopoteza mechi ya tatu pekee msimu huu jana wangeweza kuvuna mabao zaidi kama si maamuzi ya utata ya waamuzi pamoja na umakini wa washambuliaji wake ambapo ilimaliza dakika 45 ikiwa pungufu, baada ya mshambuliaji wake Mzambia, Obrey Chirwa kuoneshwa kadi mbili za njano za utata ndani ya dakika mbili na kutolewa kwa kadi nyekundu dakika ya 45.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako