• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa lalaani vikali mashambulizi ya mabomu nchini Afghanistan

    (GMT+08:00) 2017-03-02 18:05:13

    Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limelaani vikali mashambulizi ya mabomu yaliyotokea tarehe 1 mjini Kabul, Afghanistan.

    Katika taarifa yake, Baraza hilo limesema linafuatilia kwa karibu matishio la makundi ya Taliban, Al-Qaeda, IS na makundi mengine haramu ya watu wenye silaha dhidi ya raia na jeshi nchini Afghanistan. Pia Baraza hilo limesisitiza kuwa ni lazima watekelezaji, wapangaji, wafadhili na waungaji mkono wa vitendo vya kigaidi wachukuliwe hatua za kisheria, na linatoa mwito kuzitaka nchi mbalimbali kupambana na ugaidi kwa nguvu zote. Taarifa hiyo pia inasema, vitendo vyovyote vya kimabavu na kigaidi haviwezi kuzuia mchakato wa kutimiza amani, demokrasia na utulivu nchini Afghanistan ambao unaongozwa na watu wake.

    Milipuko miwili ilitokea jana mjini Kabul na kusababisha vifo vya watu wasiopungua 16, wakiwemo wanawake na watoto.

    Kundi la Taliban limetangaza kuhusika na mashambulizi hayo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako