• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Jeraha la kichwa la Fernando Torres lashtua mashabiki na wachezaji wa Atletico Madrid

    (GMT+08:00) 2017-03-03 09:17:46

    Staa wa soka wa kimataifa wa Hispania anayeichezea Atletico Madrid Fernando Torres jana usiku aliwawacha kinywa wazi mashabiki wa soka na wachezaji wenzake kufuatia kupata jeraha la kichwa na kufanya kila mchezaji aliyepo uwanjani kushituka kwa jeraha hilo.

    Torres ambaye alikuwa sehemu ya kikosi cha Atletico Madrid kilichocheza na Deportivo la Coruna na mchezo kumalizika kwa sare ya 1-1, alilazimika kukimbizwa hospitali na gari la wagonjwa kufuatia kuumia kichwani na kupoteza fahamu baada ya kugongwa na Alex Bergantinos dakika ya 85.

    Taarifa kutoka hospital ambapo nyota huyo wa zamani wa Liverpool na Chelsea aliyezichezea timu hizo kwa nyakati mbili tofauti, amepata fahamu na Atletico wameripoti kuwa kwa sasa atakuwa katika uangalizi wa daktari.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako