• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Baraza la Seneti la Marekani laidhinisha uteuzi wa Rick Perry kuwa waziri wa nishati

    (GMT+08:00) 2017-03-03 16:38:29

    Baraza la Seneti nchini Marekani limeidhinisha uteuzi wa Rick Perry aliyependekezwa na rais Donald Trump kuwa waziri wa nishati kwa kura za ndio 62 dhidi ya 37 za hapana.

    Bw. Perry mwenye umri wa miaka 66 alikuwa gavana wa jimbo la Texas kuanzia mwaka 2000 hadi 2015. Kwenye kampeni yake ya kuwania uteuzi wa mgombea urais wa chama cha Republican mwaka 2012, aliwahi kutaka kufutwa kwa wizara ya nishati.

    Watetezi wa mazingira wanampinga Perry kuwa waziri wa nishati wakidai kuwa yeye anatia mashaka kuhusu shughuli za binadamu kusababisha mabadiliko ya hali ya hewa, na pia ana uhusiano wa karibu na sekta ya mafuta na gesi jimboni Texas.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako