• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Ukame na mvua kubwa kuathiri maisha mashariki na kusini mwa Afrika.

    (GMT+08:00) 2017-03-03 17:11:59

    Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa (FAO) limesema karibu nchi 37 zinahitaji msaada wa chakula toka nje, zikiwemo nchi 28 za Afrika, kutokana na kuenea kwa athari za mvua za El-nino za mwaka jana ambazo zimesababisha ukame kwenye sekta ya kilimo .

    Nchini Sudan Kusini, karibu nusu ya watu wote milioni 11.3 wanahitaji msaada wa dharura wa chakula baada ya Umoja wa Mataifa kutangaza kuwepo njaa katika nchi hiyo wiki iliyopita.

    Nchini Somalia, mashirika 44 ya msaada ya kitaifa na kimataifa yametoa ombi kwa Umoja wa Mataifa kuchukua hatua za haraka kuzuia njaa inayoweza kutokea katika nchi hiyo ambako watu wasiopungua milioni 6.2 wanakabiliwa na uhaba wa chakula.

    Wakati huohuo katika nchi ya kusini mwa Afrika Zimbabwe, serikali imetangaza hali ya maafa ikisema watu 264 wamekufa na wengine elfu 2 kupoteza makazi wakati mvua kubwa zinaendelea kusababisha mafuriko.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako