• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Nchi tano kunufaika kibiashara kutokana na huduma za meli katika ziwa Nyasa

    (GMT+08:00) 2017-03-03 19:35:56

    Biashara kati ya Zambia, Tanzania, Jamhuri ya kidemokrasia ya Kongo,Afrika Kusini na Malawi inaelekea kuwa na mafanikio baadfa ya kupata huduma mpya baada ya meli mbili mpya kufanya majaribio katika ziwa Nyasa mkoani Mbeya. Akizungumza na radio China kimataifa, Kaimu mkuu wa bandari ya Itungi-Kyela Bwana Ajuaye Msese amesema kama majaribio ya meli hizo yatakamilika na meli hizo kuthibitishwa kuwa salama basi wananchi wa pande zote watapata fursa ya kuendesha shughuli zao za kibiashara bila matatizo yoyote.Meli hizo mbili za mizigo ambazo zilitengenezwa na kampuni ya Songoro Marine tayari zimeshushwa katika ziwa hilo kwa ajili ya majaribio. Meli hizo ni kati ya tatu ikiwemo ile ya abiria ambazo kwa ujumla zimejengwa kwa gharama ya shilingi bilioni 20.Kila meli itakuwa na uwezo wa kubeba tani 1,000 ya mizigo tofauti tofauti.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako