• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Matukio makubwa yaliyotokea wiki hii (25 Feb- 3 Machi)

    (GMT+08:00) 2017-03-03 19:56:23

    Jeshi la Kenya lauwa wapiganaji 57 wa kundi la kigaidi la Al Shabaab

    Jeshi la Kenya limesema kuwa wameua wapiganaji 57 wa kundi la kigaidi la Al Shabaab katika mapambano huko kusini mwa Somalia mapema wiki hii.

    Waziri wa ulinzi wa Kenya amesema kuwa Vikosi chini ya majeshi ya umoja wa Africa (amisom) vilitumia mashmbulizi ya anga dhidi ya waasi hao karibu na mji wa Afmadow, takribani kilomita 100 kaskazini magharibi mwa Kismayo.

    Lakini Al-Shabaab walikana juu ya taarifa hiyo ya kuuawa kwa wapiganaji wake.

    Ripoti nyingine kutoka kambi ya wakimbizi ya Dadaab, iliyo kaskazini mashariki mwa Kenya, inasema kuwa walimu wawili raia wa Kenya wametekwa nyara.

    Walimu hao walivamiwa manyumbani mwao na watu wenye silaha na wanaaminiwa kusafirishwa kuenda mpaka wa Somalia.

    Walimu hao wanatajwa kuwa wasio na asili ya Somalia na walikuwa wakifunza kwenye shule moja ya kibinafsi iliyo kambi ya wakimbizi ya Hagardheere ambayo ni moja ya kambi za Dadaab.


    1 2 3 4 5 6 7
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako