• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Matukio makubwa yaliyotokea wiki hii (25 Feb- 3 Machi)

    (GMT+08:00) 2017-03-03 19:56:23

    Taharuki yatanda Afrika Kusini kufuatia wenyeji kuwashambulia wageni

    Wiki hii nchini Afrika kusini hali ya taharuki imeendelea kushuhudiwa kufuatia wenyeji kuwashambulia wageni

    Msemaji wa Polisi wa jimbo la Gauteng nchini Afrika Kusini Kanali Lungelo Dlamini, amesema watu watano walikamatwa wiki hii mjini Johannesburg kwa kuvamia maduka na kufanya vurugu.

    Polisi wa Afrika Kusini waliwasindikiza wageni nje ya mji wa Jeppestown baada ya kutishiwa Jumatatu usiku.

    Polisi hao walilazimika kuingilia kati baada ya wakazi wenye chuki dhidi ya wageni kuanza kupora maduka ya wageni kwenye eneo hilo, polisi walilazimika kutumia maguruneti na risasi za mpira.

    Kanali Dlamini amesema polisi wamewaonya wananchi wanaofanya uhalifu huo kuwa vitendo vyao havitavumiliwa.

    Aidha amewataka watu kuripoti matukio ya vitisho, vurugu na uporaji kwenye vituo vya polisi vya karibu.

    Wakati huo huo Wizara ya mashauri ya nchi za kigeni nchini Afrika Kusini imethibitisha ripoti kuwa raia kadha wa Nigeria wamefukuzwa kutoka nchini humo kwani wanaishi huko kinyume cha sheria.

    Afrika Kusini imekumbwa na ghasia dhidi ya raia wa kigeni na visa vya kuporwa kwa maduka yanayomilikiwa na wahamiaji.


    1 2 3 4 5 6 7
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako