• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China yaweka lengo la ukuaji wa uchumi kwa mwaka 2017 kuwa wa asilimia 6.5

    (GMT+08:00) 2017-03-05 10:02:45

    China imeweka lengo la pato la taifa GPD kuwa asilimia 6.5 kwa mwaka huu, kiasi ambacho ni cha chini zaidi katika miaka 25 iliyopita, na pia ni cha chini kuliko asilimia 6.7 ya ukuaji wa uchumi wa China katika mwaka jana.

    Kwa mujibu wa ripoti ya kazi za serikali iliyotolewa leo na waziri mkuu wa China Li Keqiang kwenye mkutano wa mwaka wa Bunge la Umma la China, lengo hilo linalingana na kanuni za kiuchumi na halisi, na kwamba litasaidia kutuliza matarajio ya soko na kurahisisha mabadiliko ya kimuundo nchini humo. Pia litasaidia kufanikisha lengo la kujenga jamii yenye maisha mazuri katika pande zote.

    Ripoti hiyo pia imesema, sababu muhimu ya kusisitiza hitaji la kudumisha ukuaji tulivu ni kuhakikisha soko la ajira na kuinua kiwango cha maisha ya watu. Lengo la mwaka huu kwa utengenezaji wa nafasi za ajira mijini ni zaidi ya milioni 11, ambayo ni ongezeko la milioni 1 kuliko mwaka jana.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako