• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais wa Marekani alitaka bunge kuchunguza kama serikali ya Obama ilitumia ovyo haki ya uchunguzi

    (GMT+08:00) 2017-03-06 09:07:42

    Ikulu ya Marekani jana imetoa taarifa ikisema rais Donald Trump amelitaka bunge la nchi hiyo kuchunguza kama serikali ya Obama ilitumia ovyo haki ya uchunguzi kwenye kipindi cha uchaguzi mkuu mwaka jana. Jumamosi asubuhi rais Trump kwenye ukurasa wake wa Twitter aliilaani serikali ya Obama kwa kufanya udukuzi kwenye ofisi yake mjini New York tarehe 8 Novemba mwaka jana kabla ya upigaji kura. Msemaji wa Barack Obama alitoa taarifa akikanusha tuhuma hizo na kusisitiza kuwa kanuni muhimu ya serikali ya Obama ilikuwa maofisa wa ikulu kutoingilia uchunguzi huru unaoongozwa na wizara ya sheria.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako