• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • EPL, Wenger lawamani tena, huku Manchester United ikisalia nafasi ya 6

    (GMT+08:00) 2017-03-06 10:18:22
    Licha ya kulaumiwa mno kwa uamuzi wake wa kumuweka benchi staa wake Alexis Sanchez kwenye mechi kadhaa, Arsenal walitwangwa 3-1 huko Anfield na Liverpool.

    Meneja wa Arsenal Arsene Wenger ametetea uamuzi wake huo wa kutomuanzisha Sanchez. Wakiwa 2-0 nyuma, Wenger alimuingiza Sanchez wakati wa Haftaimu na yeye ndio alietoa Pasi ambayo Danny Welbeck aliifungia Arsenal bao lao moja.

    Baada ya Mechi hiyo, Wenger alieleza kuwa alitaka kuwaanzisha Wachezaji ambao ni wazuri kwa Mipira ya juu na kisha kumuingiza Sanchez Kipindi cha Pili.

    Huku nako Manchester United imesalia katika nafasi ya 6 baada ya kupata sare ya 1-1 dhidi ya wageni wao Bournemouth ambao walicheza wakiwa wachezaji 10 uwanjani. Matokeo mengine ya ligi hiyo Tottenham Spurs na Manchester City zimejichimbia nafasi ya 2 na ya 3 baada ya jana kushinda mechi zao za Ligi hiyo.

    Spurs, wakicheza kwao White Hart Lane, waliifunga Everton 3-2 na kujiweka vizuri nafasi ya Pili wakiwa na Pointi 56 kwa Mechi 27 huku kileleni wapo Chelsea wenye Pointi 63 kwa Mechi 26.

    Huko Stadium of Light, Sunderland wamebaki mkiani baada ya jana kuchapwa 2-0 na Man City kwa bao za Sergio Aguero na Leroy Sane.

    Ushindi huu umewaweka Man City nafasi ya 3 wakiwa na Pointi 55 kwa Mechi 26.

    Ligi hiyo inaendelea tena leo ambapo vinara wa ligi hiyo Chelsea watakapovaana na West Ham United.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako