• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • La Liga: Barca yapiga 5, huku Real wafunga 4

    (GMT+08:00) 2017-03-06 10:18:44

    Mabingwa Watetezi wa La Liga Barcelona jana usiku waliitwanga Celta Vigo 5-0 uwanjani Nou Camp na kurejea kileleni mwa Ligi hiyo baada ya mapema hiyo Jana Real Madrid kuifunga Eibar 4-1 na kukalia kiti hicho.

    Barca wapo kileleni kwa Pointi 1 zaidi ya Real lakini wao Barca wamecheza Mechi 1 zaidi.

    Bao za Barca zilipachikwa na Lionel Messi, Bao 2, Neymar, Rakitic na Umtiti.

    Nao Real Madrid wakicheza Ugenini na Eibar bila ya Staa wao mkubwa Cristiano Ronaldo na pia kuwakosa Mastraika wao wengine Gareth Bale na Alvaro Morata walishinda Mechi hiyo 4-1.

    Bao za Real zilifungwa na Karim Benzema, Bao 2, Rodriguez na Asensio huku Bao pekee la Eibar likipigwa na Pena.

    Ligi hiyo inaendelea leo kati ya timu ya Deportivo Alaves na Sevilla.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako