• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kenya:Mzozo wa mifugo wazidi kuchangia hasara

    (GMT+08:00) 2017-03-07 19:10:53

    Wafugaji 379 wamekamatwa kufuatia kifo cha mmoja wa wakurugenzi wa hifadhi ya wanyama ya Sosian, Tristan Voorspuy, katika kaunti ya Laikipia.

    Serikali imesema kuwa mauaji hayo yalitokana na wafugaji haramu wanaovamia hifadhi za wanyama za watu binafsi kutafuta lishe za mifugo yao huku hali ya ukame ikiiendelea kuathiri kaunti hizo.

    Katika taarifa iliyotiwa saini kwa pamoja na mawaziri Joseph Nkaisserry wa usalama wa kitaifa, Najib Balala wa Utalii na Judy Wakhungu wa mazingira, serikali ilithibitisha kuwa mkurugenzi wa idara ya upelelezi, Ndegwa Muhoro, yuko katika eneo la Laikipia kuzindua uchunguzi kuhusiana na mauaji hayo.

    Ilichukuwa saa kadhaa kwa mwili wake kuondolewa kwa hofu kuwa washambuliaji hao bado walikuwa wamejificha katika vichaka. Siku ya Jumamosi, helikopta ya polisi ilipigwa risasi katika shamba hilo wakati maafisa wa usalama walipotekeleza ukaguzi wa angani mahali ambapo wafugaji haramu na wakora wamekuwa wakiendeleza uharibifu.

    Ripoti za awali zinaashiria kuwa inspekta jenerali wa polisi alikuwa katika helikopta hiyo iliyokuwa imelengwa lakini alikanusha ripoti hizo na kusema kuwa tayari alikuwa ameondoka katika eneo hilo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako