• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Sudan, UNDP wazindua mradi wa kupambana na vurugu za siasa kali

    (GMT+08:00) 2017-03-10 09:10:44

    Kamati ya taifa ya kupambana na ugaidi ya Sudan kwa ushirikiano na Shirika la mipango ya maendeleo la Umoja wa mataifa UNDP wamezindua mradi wa kupambana na vurugu za siasa kali (PAVE) nchini Sudan.

    Wawakilishi wa serikali, wajumbe wa kamati, maofisa wa umoja wa mataifa, wahisani, taasisi zisizo za kiserikali, viongozi wa kidini, na makundi ya vijana walishuhudia uzinduzi wa mradi huo.

    Waziri Mkuu na makamu wa kwanza wa Rais wa nchi hiyo Bw Bakri Hassan Saleh alihudhuria uzinduzi wa mradi huo, na kusisitiza nia ya serikali ya Sudan Kusini kushirikiana kwenye mapambano dhidi ya siasa kali.

    Mratibu wa misaada ya kibinadamu na mwakilishi wa UNDP nchini Sudan Bibi Marta Ruedas amesema vurugu za siasa kali sio tu zinaiathiri Sudan, bali pia zinaathiri dunia nzima. Ameipongeza serikali ya Sudan kwa juhudi za kupambana na tatizo hilo, na hasa kuangalia vyanzo vyake.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako