• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mbwana Samatta wa KRC Genk aondoa ukame wa magoli

    (GMT+08:00) 2017-03-10 09:32:58

    Nahodha wa timu ya taifa ya Tanzania Mbwana Samatta akiwa na timu yake ya KRC Genk walikuwa ugenini kucheza mchezo wao wa kwanza hatua ya 16 bora wa UEFA Europa League dhidi ya KAA Gent, kutoka Ubelgiji. Samatta anarudi katika historia tena kwa kuondoa ukame wa magoli baada ya kufanikiwa kuifungia magoli mawili KRC Genk katika ushindi wa maoli 5-2. Mbwana Samatta anafunga magoli hayo mawili katika mechi yake ya 9 ya Europa League toka waingie katika hatua ya makundi na alikuwa hajafunga goli lolote. Magoli ya Genk yalifungwa na Ruslan Malinovsky dakika ya 21, Omar Colley dakika ya 33, Mbwana Samatta dakika ya 41 na 72 na Jere Uronen dakika ya 45. KAA Gent ambao watalazimika kuifuata KRC Genk katika mchezo wa marudiano March 16 2017, magoli yao mawili yalifungwa na Samuel Kalu dakika ya 27 na Kalifa Coulibaly dakika ya 61, ushindi huo unawapa Genk matumaini zaidi ya asilimia 50 kucheza robo fainali kwani ili watolewe KAA Gent italazimika kushinda kwa magoli 4-0 mchezo wa marudiano.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako