• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China yatoa msaada wa dola za kimarekani milioni moja kwa wakimbizi wa Afghanistan

    (GMT+08:00) 2017-03-10 17:16:20

    Serikali ya China imelikabidhi Shirika la kuhudumia wakimbizi la Umoja wa Mataifa UNHCR dola za kimarekani milioni moja ambazo zitatumika kutoa msaada wa kibinadamu kwa wakimbizi nchini Afghanistan.

    Kwa mujibu wa makubaliano husika, UNHCR litawakilisha serikali ya China kununua, kusafirisha na kupanga misaada husika.

    Balozi wa China nchini Afghanistan Bw. Yao Jing ameeleza matumaini yake kuwa msaada huo unaweza kusuluhisha msukosuko wa kibinadamu nchini Afghanistan.

    Kwa niaba ya serikali ya Afghanistan, waziri wa wakimbizi na huduma za urudishaji wa wakimbizi wa Afghanistan Bw. Syed Balkhi ameishukuru serikali ya China kwa msaada huo na kusema, ni ishara ya urafiki mkubwa kati ya serikali za nchi hizo mbili na wananchi wao.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako