• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Wachina wanaoishi Kenya watoa msaada wa chakula kwa waliokumbwa na ukame

    (GMT+08:00) 2017-03-13 10:10:53

    Jumuiya ya wachina wanaoishi nchini Kenya wametoa msaada wa chakula kwa watu wanaokabiliwa na ukame mashariki mwa nchi hiyo.

    Ukame huo ambao pia umezikumba nchi za jirani za Somalia na Sudan Kusini umeathiri zaidi ya watu milioni 6.

    Msaada huo umetolewa kwa ajili ya wakazi wa eneo la Kaiti kaunti ya Makueni, ambayo kwa muda wa misimu miwili haikuwa ya kutosha kuwawezesha wakulima kupata mavuno, na sasa wakazi wameanza kushuhudia makali ya njaa.

    Msaada huo ni pamoja na tani 30 za vyakula kama vile Unga wa ngano na mahindi, biskuti na mafuta ya kupikia na maji ya kunywa.

    Maeneo yaliyoathiriwa zaidi na ukame ni kaunti za Taita Taveta, Kilifi na Kwale na maeneo ya Mashariki ya Nchi.

    Tayari serikali imeitangaza njaa na ukame kuwa janga la kitaifa huku mvua ikitarajiwa baadaye mwezi huu.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako