• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Jeshi la Iraq lakaribia kuingia katikati ya mji wa Mosul

    (GMT+08:00) 2017-03-13 18:15:40

    Serikali ya Iraq imedhibiti zaidi ya theluthi moja ya eneo la magharibi mwa mji wa Mosul baada ya mapambano ya wiki nne ambayo yaliliwezesha jeshi la nchi hiyo kukaribia eneo kongwe la mji huo na kuzuia njia zote za kutoroka kwa wapiganaji wa kundi la IS mjini humo.

    Luteni Jenerali Abdul-Amir Yarallah anayeongoza operesheni ya pamoja ya mapambano dhidi ya IS nchini Iraq amesema polisi na vikosi vya operesheni hiyo vinasonga mbele kwenye eneo kongwe lililo magharibi mwa Mosul huku vikosi vya kupambana na ugaidi vikifanikiwa kudhibiti eneo jipya la Mosul .

    Wakati huo huo, jeshi la Iraq limepata maendeleo katika eneo la kaskazini magharibi mwa mji huo, na kukata njia ya mwisho inayotumiwa na wapiganaji wa kundi la IS kutoroka mjini humo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako