• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China yazihimiza tena pande mbili za suala la peninsula ya Korea kusimamisha shughuli zao

    (GMT+08:00) 2017-03-13 18:51:55

    Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya China Bibi Hua Chunying amesema hali ya sasa katika peninsula ya Korea ni nyeti na ina utatanishi mkubwa, pande husika zinatakiwa kutuliza mvutano huo na kulinda amani na utulivu wa kanda hiyo.

    Hua amesema hayo alipokuwa akizungumzia luteka ya pamoja ya kijeshi iliyoanza leo kati ya Korea Kusini na Marekani. Bi. Hua amesisitiza tena mapendekezo yaliyotolewa na China kwamba pande husika zinatakiwa kushikilia kanuni ya kuifanya peninsula hiyo iwe sehemu isiyo na silaha za nyuklia na kubadilisha mfumo wa kusimamisha vita kuwa mfumo wa kutimiza amani. Pia amesema Korea Kaskazini inatakiwa kusimamisha majaribio ya nyuklia na makombora, na Marekani na Korea Kusini pia zinatakiwa kusimamisha kufanya luteka kubwa.

    Wakati huohuo, Bibi Hua pia amesema mjumbe maalum wa serikali ya China anayeshughulikia mambo ya Latin Amerika Balozi Yin Hengmin atahudhuria mazungumzo ya ngazi ya juu ya mafungamano ya kiuchumi ya eneo la Asia na Pasifiki huko Chile tarehe 14 hadi 15, lakini amesisitiza kuwa mkutano huo si mkutano wa Ushirikiano wa kibiashara na Nchi za Pasifik (TPP) kama baadhi ya vyombo vya habari vilivyosema.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako