• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kenya: bei ya kahawa imepanda kidogo katika mnada wa Nairobi

    (GMT+08:00) 2017-03-13 19:29:37

    Bei ya kahawa katika mnada wa Nairobi mnada imerudi kidogo kwa hali ya kawaida katika mauzo ya wiki iliyopita baada ya kupungua kwa asilimia 17 katika biashara ya wiki iliyotangulia.

    Ripoti ya Soko kutoka mnada wa kahawa Nairobi (NCE) inaonyesha kwamba mfuko wa kilo 50 wa kahawa iliuzwa kwa Sh27,030 wiki iliyopita ikilinganishwa na Sh26,059 katika mauzo ya mbeleni.

    Mwelekeo mpya ya bei ya chini katika mnada unatokana na maharage ya viwango vya chini.

    Daniel Mbithi, mtendaji mkuu wa NCE, anasema kuna uwezekano wa kuboreka kwa bei katika mauzo ijayo kutokana na kuongezeka kwa mazao ya viwango vya chini ambayo imepunguza kasi ya mahitaji.

    Bw Mbithi anasema inatarajiwa kwamba bei za chini zitashuhudiwa katika mwezi wa Machi kutokana na viwango vya chini vya maharagwe ambazo zitaanza kuingia katika soko.

    Mapato ya kahawa yaliboreka kwa asilimia 63 mwezi uliopita ikilinganishwa na kipindi kama hicho mwaka 2016 kutokana na bei ya juu ya kimataifa na kuongezeka kwa wingi wa kahawa katika mnada wa Nairobi.

    Takwimu kutoka NCE zinaonyesha kuwa thamani ya kahawa ya Kenya iliyouzwa mwezi uliopita ilifikia Sh bilioni 9.3 ($ 90,970,000) ikilinganishwa na Sh bilioni 5.7 bilioni ($ 55,510,000) iliyouzwa mwezi Februari 2016.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako