• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais Kenyatta azindua huduma za feri katika kivuko cha Mtongwe

    (GMT+08:00) 2017-03-14 10:39:46

    Rais Uhuru Kenyatta amezindua i kivuko cha Mtongwe kusini mwa mji wa Mombasa baada ya miaka kadhaa ya mateso kwa wakazi wanaotumia kivuko hicho.

    Akiongea kwenye uzinduzi huo rais Kenyatta amesema kivuko hicho kitaweza kuhudumia takriban wakazi elfu 30 kwa siku. Amesema serikali yake imetenga Sh2.2bilioni za Kenya kwa ajili ya kununua feri mbili mpya ili kuboresha huduma sehemu hiyo.

    Kivuko cha Mtongwe kilisitisha kutoa huduma mwaka 2011 baada ya serikali kusema kimechakaa.

    Masuala hayo ya kiusalama yaliafikiwa kufuatia ajali mbaya ya feri iliyotokea tarehe 29 Aprili mwaka 1994 ambapo feri ya MV Mtongwe ilizama na takriban watu 270 kupoteza maisha yao na wengine 190 kujeruhiwa.

    Rais Kenyatta alitangaza kuwa vivuko vipya viwili vitawasili Kenya kati ya mwezi Juni na Julai mwaka huu, ikiwa ni sehemu ya mipango ya serikali ya kurahisisha uvukaji wa watu na mizigo kuelekea kusini mwa pwani ya Kenya.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako