• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Uzalishaji wa kiviwanda nchini China waongezeka kwa asilimia 6.3 kwa miezi ya Januari na Februari

    (GMT+08:00) 2017-03-14 17:04:16

    Mamlaka ya Takwimu ya China NBS imesema, uzalishaji katika sekta ya viwanda nchini China umeongezeka kwa asilimia 6.3 katika miezi miwili ya mwanzo ya mwaka huu, ikilinganishwa na ongezeko la asilimia 6 la mwezi Disemba mwaka jana.

    Mamlaka hiyo imesema, ongezeko hilo ni la juu zaidi kuliko ongezeko lililopatikana mwaka jana la asilimia 6.

    Uchumi wa China ulikua kwa asilimia 6.7 mwaka jana, ikiwa ni ukuaji wa kasi ya chini zaidi katika miaka 26 iliyopita, lakini ikiwa ndani ya malengo yaliyowekwa na serikali. Lengo la ukuaji wa uchumi kwa mwaka huu nchini China limewekwa kuwa karibu asilimia 6.5, au zaidi, huku likitoa nafasi ya kutosha kwa ajili ya mageuzi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako