• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China yatekeleza kithabiti utaratibu uliopo duniani wa kupambana na dawa za kulevya

    (GMT+08:00) 2017-03-14 19:06:41

    China inalinda kithabiti utaratibu uliopo sasa duniani wa kupambana na dawa za kulevya na kupenda kushiriki kwenye ushirikiano wa kimataifa katika suala hilo.

    Hayo yamesemwa na naibu katibu mkuu mtendaji wa kamati ya kupambana na dawa za kulevya ya China Liang Yun kwenye mkutano wa 60 wa Tume ya Dawa za Kulevya CND ya Umoja wa Mataifa unaofanyika mjini Vienna. Amesema China inapendekeza kutekelezwa bila tatizo utaratibu wa kimataifa wa kupambana na dawa za kulevya unaotekelezwa hivi sasa, kuimarisha utekelezaji wa mikataba mitatu ya kimataifa, na kulinda hadhi ya Tume ya CND katika kutunga sera husika.

    Ameongeza kuwa katika mwaka uliopita, China imepambana na dawa za kulevya kwa kanuni ya kuzingatia pande zote, ya jumla na uwiano, kujitahidi kushiriki kwenye ushirikiano wa kimataifa, na kutoa mchango kwa utatuzi wa suala la dawa za kulevya duniani.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako