• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rwanda:Rwanda yalenga kukusanya ushuru zaidi.

    (GMT+08:00) 2017-03-14 18:57:11

    Washauri wa masuala ya ushuru nchini Rwanda wametakiwa kubuni mbinu za kuongeza ukusanyaji wa ushuru kutoka kwa wafanyibiashara.

    Martin Nkurunzinza mwenyekiti wa chama cha washauri wa ulipaji ushuru amesema kuna haja ya wadau hao kuongeza juhudi za kuwafikia walipaji ushuru ili kuhakikisha mapato yanaongezeka.

    Kwa sasa halmashauri ya ushuru imeanzisha mkutano maalum wa kujadili namna ya kuwakamata wakwepaji ushuru kwa kutumia mfumo wa elektroniki.

    Bodi ya ushuru imeanzisha mafunzo katika kila mkoa nchini Rwanda kutoa ujuzi kwa maafisa wa wake kuhusiana na kugundua wanaokwepa ushuru.

    Elimu ya umma kuhusiana na ulipaji ushuru aidha imeanzishwa kote Rwanda kuhamasisha watu kulipa ushuru.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako