• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rwanda:Wakulima wahimizwa kupanda ngano

    (GMT+08:00) 2017-03-14 18:57:54

    Bodi ya wakulima nchini Rwanda imetoa mwito kwa wakulima nchini humo kuongeza uzalishaji wa ngano ili kutimiza mahitaji ya nchi hiyo.

    Mkurugenzi wa bodi hiyo Cyubahiro Bagabe amesema wakulima wanatakiwa kutumia mbegu bora za kuhimili ukame na upepo.

    Lengo la nchi hiyo ni kupanda tani 4 kwa kila hekari kutoka tani 2 kwa kila hekari.

    Wizara ya kilimo inalenga kufikia tani 9600 za ngano kufikia mwaka 2019.

    Kulingana na maafisa wa bodi ya kilimo ya Rwanda ,uzalishaji wa kutosha wa ngano utapunguza hali ya sasa ya nchi hiyo kutegemea ngano kutoka nchi jirani.

    Rwanda kwa sasa inanunua ngano na kutayaraisha kutoka kwa kapmuni ya Pembe ya Kenya.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako