• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Naibu waziri mkuu wa China kufanya ziara nchini Ufilipino

    (GMT+08:00) 2017-03-14 19:18:38

    Naibu waziri mkuu wa China Wang Yang anatarajiwa kufanya ziara rasmi nchini Ufilipino kuanzia Alhamisi hadi Jumapili wiki hii, ambapo atakutana na rais Rodrigo Duterte wa nchi hiyo.

    Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya China Hua Chunying amesema inaaminika kuwa ziara hiyo inaweza kuhimiza zaidi ushirikiano wa kimkakati kati ya China na Ufilipino unaolenga kusukuma mbele amani na maendeleo kati yao. Wakati wa ziara hiyo, mbali na kukutana na rais Duterte, Bw. Wang pia atakutana na kundi la masuala ya uchumi la baraza la mawaziri la Ufilipino, kuhudhuria uzinduzi wa mwaka wa ushirikiano wa kitalii kati ya China na Jumuiya ya Nchi za Asia Kusini Mashariki ASEAN, na ufunguzi wa kongamano la uchumi na biashara kati ya nchi hizo mbili.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako