• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kenya Mpango wa majaribio wa uzalishaji wa mafuta mwezi Aprili unaanza

    (GMT+08:00) 2017-03-15 19:35:02

    Mpango wa majaribio na Kenya kuanza kusafirisha mafuta ghafi kutoka mashamba ya mafuta Turkana imeanza kuonekana kuwa karibu na kweli.

    Wizara ya Nishati na Petroli jana ilitia saini kwa mkataba na Tullow Oil, Africa Oil Mafuta na Maersk Oil.

    Mkataba huu umetangeneza njia kwa kampuni hizi tatu, kuendelea na mpango wa mapema wa majaribio ifikapo mwezi ujao.

    Makampuni ya mafuta ambayo yameshiriki katika utafiti wa mafuta katika Kaunti ya Turkana, wamesema watanza uzalishaji wa mapipa 2,000 ya mafuta kwa siku ifikapo mwezi Aprili.

    Waziri wa Nishati na Petroli Charles Keter amesema makampuni hayo matatu yalikuwa yametia saini mkataba wa makubaliano na Kenya Petroleum Refineries Ltd (KPRL) kwa ajili ya kuhifadhi ya mafuta ghafi katika kituo chake mjini Mombasa kabla ya kusafirisha nje.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako