• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rwanda:Benki ya AFDB kutoa ajira kwa vijana Afrika

    (GMT+08:00) 2017-03-15 19:36:13

    Benki ya maendeleo ya Afrika (Afdb Bank)imetangaza mpango wake wa kuwatafutia ajira vijana na kuhakikisha bara la Afrika lina chakula cha kutosha.

    Katika ripoti yake kwa vyombo vya habari,benki hiyo imesema itashirikiana na benki nyingine 5 duniani kuweka miradi ya kilimo katika nchi zote za bara la Afrika.

    Mradi huo wa jina lisha Afrika utaanzishwa mwaka huu hadi 2025 katika lengo la kumaliza umaskini na ukosefu wa chakula pamoja na kukabiliana na maradhi ya utapia mlo.

    Kupitia kwa bodi yake ya ubunifu wa miradi ya ajira benki hiyo imetangaza kuweka miradi ya kubuni nafasi milioni 25 za ajira kwa vijana milioni 50barani Afrika kupitia biashara tofauti.

    Taarifa ya usimamizi wa benki hiyo imesema wanataka kuhakikisha vijana hawategemei kuajiriwa na kampuni na mashirika ya kazi pekee bali kujitegemea wenyewe kupitia kwa vipaji vyao na ubunifu.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako