Michezo miwili ya mwisho ya hatua ya 16 bora ya marudiano kwenye michuano ya klabu bingwa Ulaya UEFA msimu wa 2016/2017 ilichezwa usiku wa March 15 2017, ambapo Man City walisafiri kwenda kucheza na AS Monaco Ufaransa huku Atletico Madrid wakiwa wenyeji wa Bayer Lerkusen ya Ujerumani.
Kwa upande wa Man City bahati haikuwa yao baada ya kuaga michuano hiyo kwa kukubali kipigo cha magoli 3-1 hivyo wanaondolewa kwa sheria ya magoli ya ugenini ya 6-6 kutokana na kuruhusu kufungwa magoli mengi nyumbani. Nayo Atletico Madrid inafuzu kwa kuifunga Bayer kwa sheria ya magoli ya ugenini ya 4-2 licha ya mchezo huo wa jana kumaliza kwa sare tasa 0-0.
Michezo hiyo ndio iliyofunga hatua ya 16 bora ya michuano ya klabu bingwa Ulaya msimu wa 2016/2017, kwa sasa michuano hiyo inaingia hatua ya robo fainali, ratiba kamili ya hatua ya robo fainali itafahamika kesho Ijumaa baada ya kuchezeshwa droo.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |