• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • FA yapitisha rungu lake kwa Manchester United

    (GMT+08:00) 2017-03-16 09:21:38
    Klabu ya Manchester United imeshtakiwa na shirikisho la soka nchini Uingereza FA kwa kushindwa kuwadhibiti wachezaji wake wakati wa mechi ya robo fainali ya kombe la FA siku ya Jumamosi dhidi ya Chelsea.

    Refa Michael Oliver alizungukwa na wachezaji wa United baada ya kumpa kadi nyekundu Ander Herrera dakika 10 kabla ya muda wa mapumziko. United ilipoteza mechi hiyo kwa 1-0. Taarifa ya FA iliipa United hadi saa kumi na mbili jioni jana kwa saa za Uingereza kujibu.

    Kiungo wa kati wa Uhispania Herrera alitolewa nje baada ya kumchezea vibaya kwa mara ya pili mshambuliaji Eden Hazard. Hakuna hatua zaidi itakayochukuliwa dhidi ya Marcos Rojo akwa kosa alilofanya katika dakika za mwisho za mechi. Rojo alionekana akimkanyaga Hazard.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako