• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Viongozi wa China na Saudi Arabia wakubaliana kinua zaidi uhusiano kati ya nchi zao

    (GMT+08:00) 2017-03-16 18:20:11

    Rais Xi Jinping wa China leo hapa Beijing amefanya mazungumzo na mfalme Salman bin Abdulaziz Al Saud wa Saudi Arabia.

    Viongozi hao wamekubaliana kudumisha mwelekeo wa maendeleo ya uhusiano kati ya China na Saudi Arabia, kusukuma mbele ushirikiano katika pande mbalimbali, na kusukuma mbele uhusiano wa wenzi wa kimkakati kati ya nchi hizo mbili.

    Rais Xi Jinping amesema China inaunga mkono Saudi Arabia kutimiza "dira ya mwaka 2030", na inaipongeza Saudi Arabia kuwa mwenzi wa China katika ujenzi wa "Ukanda Mmoja na Njia Moja", na kupenda kuwa mwenzi wa kiuchumi wa Saudi Arabia.

    Baada ya mazungumzo yao, wakuu hao wameshuhudia kusainiwa kwa nyaraka mbalimbali za ushirikiano wa sekta za uchumi, nishati, uzalishaji wa kiviwanda, utamaduni, elimu na sayansi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako