• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China na Burundi zakubaliana kuendeleza zaidi uhusiano kati yao

    (GMT+08:00) 2017-03-16 18:01:04

    Makamu wa rais wa China Li Yuanchao leo hapa Beijing amekutana na waziri wa mambo ya nje wa Burundi Bw. Alain Aime Nyamitwe.

    Bw. Li amesema, katika miaka ya karibuni, pande hizo mbili zimeongeza uaminifu wa kisiasa na ushirikiano katika sekta mbalimbali, pia zimeelewana na kuungana mkono kwenye masuala yanayohusu maslahi makuu ya upande mwingine. Pia amesema China inatarajia kuwa pande hizo mbili zitaimarisha msingi wa kisiasa wa uhusiano kati yao, kutoa kipaumbele kwa ushirikiano kwenye sekta inayohusu maisha ya watu, kupanua mawasiliano kati ya watu wa nchi hizo, na kuendeleza zaidi uhusiano kati yao.

    Kwa upande wake, Bw. Nyamitwe amesema, Burundi inapenda kuongeza ushirikiano na China katika sekta za kilimo, miundombinu, nishati na utamaduni. Pia Burundi itashirikiana na China katika mambo ya kikanda na ya kimataifa na kuimaisha uhusiano wa kirafiki wa kunufaishana.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako