• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China iko tayari kupokea pendekezo lolote linalosaidia kuondoa mvutano kwenye Peninsula ya Korea

    (GMT+08:00) 2017-03-16 18:56:56

    China iko tayari kupokea na kukubali pendekezo lolote iwapo litasaidia kuondoa mvutano uliopo kwenye Peninsula ya Korea na kulinda amani na utulivu wa kanda hiyo.

    Hayo yamesemwa na msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya China Hua Chunying alipojibu swali la mwandishi wa habari kuhusu uwezekano wa waziri wa mambo ya nje wa Marekani Rex Tillerson kuzungumzia suala la peninsula ya Korea katika ziara yake ya hivi karibuni nchini China. Bibi Hua amesema China siku zote inashikilia kanuni za kufanya Korea Kaskazini isimaishe majaribio yake ya makombora na nyuklia sambamba na kuhimiza Marekani na Korea Kusini ziache kufanya mazoezi ya kijeshi katika kanda hiyo. Amesema msimamo huo unazingatia madai ya kila upande na kulingana na matakwa ya maazimio husika ya Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako