• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rwanda: Kiwanda cha mawe Rwanda kurahisisha ujenzi wa barabara

    (GMT+08:00) 2017-03-16 19:37:35

    Gharama ya kujenga barabaraba katika mkoa wa mashariki nchini Rwanda inatarajiwa kupungua baada kufunguliwa kwa kiwanda cha kusaga mawe na kuzalisha changarawe cha Rwamagana.

    Maneja wa mradi wa kiwanda hicho kinachotumia teknolojia ya China bwana Alex Tindimwebwa amesema kitaongezea uzalishaji wa mali gafi za ujenzi kwa bei nafuu.

    Alisema kiwanda hicho kilichochengwa kwa gharama ya franc milioni 300 kitazalisha tani 500 za mawe yaliosagwa kila siku.

    Aidha kitafungua nafasi 1,000 za ajira kwa wakaazi wa wilaya ya Rwamagana . .

    Bidhaa za ujenzi nchini Rwanda hasa chuma, saruji na mawe ni sehemu ya asilimia 10 ya bidhaa ambazo huagiziwa kutoka nje.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako