• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kenya: Nauli ya Uber Kenya yapanda

    (GMT+08:00) 2017-03-16 19:40:55

    Nauli ya kutumia huduma za kampuni ya teksi ya Uber mjini Nairobi zimepanda kufuatia shinikizo zilizowekwa na wenye magari kwa kampuni hiyo.

    Mjini Nairobi sasa malipo kwa kilomita moja yatakuwa ni shilingi 42 kutoka ile ya awali ya 35.

    Aidha bei ya chini zaidi imeongezewa hadi 300 kutoka 200.

    Mjini Mombasa kilomita moja itakuwa shilingi 42 lakini bei ya chini itakuwa 200.

    Hata hivyo mbunge wa Starehe Maina Kamanda, ambaye ni mwenyekiti wa kamati ya uchukuzi amesema wangependa nauli hiyo iongezwe hadi shilingi 60 kwa kilomita.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako