• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Ethiopia : Shirika la ndege la Ethiopia laanzisha safari Zanzibar

    (GMT+08:00) 2017-03-16 19:41:40

    Shirika la ndege la Ethiopia limeanzisha safari zake kwenda Zanzibar kwa kutumia ndege ya kisasa aina ya Airbus 350 XWB.

    Kutua kwa ndege hiyo ya Shirika la Ndege la Ethiopia `Ethiopian Airlines' kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume unatajwa ni miongoni mwa juhudi za kuimarisha sekta ya utalii na kuingiza mapato zaidi.

    Ofisa Mwandamizi wa shirika hilo la ndege aliyepo Zanzibar, Eshetu Fikadu alisema hayo muda mfupi baada ya kutua kwa ndege hiyo yenye uwezo wa kubeba abiria 315.

    Alisema kuwasili kwa ndege hiyo ya kisasa ni sehemu za juhudi za shirika hilo kupanua huduma zake na kufanya safari za uhakika kwa kutumia ndege kubwa.

    Alisema kuanza safari kwa ndege hiyo ni miongoni mwa ndoto zao kutoa huduma zake kwa kutumia ndege zenye hadhi na teknolojia ya kisasa inayokwenda na wakati.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako