• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Baraza la Kilimo Tanzania (ACT) laomba serikali kuwekeza kwenye utafiti wa alizeti

    (GMT+08:00) 2017-03-16 19:42:09

    Tanzania: Baraza la Kilimo Tanzania (ACT) limeiomba serikali kuwekeza kwenye tafiti za zao la alizeti ili kuokoa Dola za Marekani milioni 230 sawa Sh500 bilioni zinazotumika kila mwaka kuagiza mafuta ya chakula kutoka nje ya nchi.

    Akifungua mkutano wa wadau wa alizeti, jana Mwenyekiti wa baraza hilo, Dk Yusuph Sinare alisema Tanzania inatumia kiasi hicho cha fedha za kigeni wakati alizeti inastawi hata kwenye maeneo yenye ukame.

    Alisema wakati umefika kwa serikali kuwekeza katika tafiti za alizeti ili kuboresha upatikanaji wa mbegu bora zitakazoongeza uzalishaji na hivyo kujitoshereza katika mafuta ya kula .

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako