• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Shirikisho la Soka Barani Afrika CAF lapata rais mpya

    (GMT+08:00) 2017-03-17 09:04:56

    Mkutano wa 39 wa shirikisho la soka barani Afrika CAF ulifanyika jana Addis-Ababa Ethiopia. Katika mkutano huo uliojadili mambo kadhaa, pia ulifanyika uchaguzi wa Rais wa shirikisho hilo. Wagombea wa nafasi za Urais walikuwa ni Rais wa sasa wa shikisho hilo Issa Hayatou na Ahmad Ahmad wa Madagascar, katika uchaguzi huo Ahmad Ahmad amemshinda Issa Hayatou kwa kura 34 wakati Hayatou akiambulia kura 20.

    Hayatou anaondoka madarakani baada ya kutawala shirikisho la soka barani Afrika CAF kwa miaka 27, Issa Hayatou aliingia madarakani mwaka 1988 na ndio Rais wa CAF aliyetawala muda mrefu zaidi akifuatiwa na Yidnekatchew Tessema aliyetawala miaka 15.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako