• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Slaven Bilic asema ingawa ulikuwa ni umuzi mbaya kumfukuza Claudio Ranieri lakini matokeo yanathibitisha kinyume

    (GMT+08:00) 2017-03-17 09:06:15

    Meneja wa West Ham, Slaven Bilic, amesema ulikuwa uamuzi ''mbaya'' kwa klabu ya Leicester City kumpiga kalamu Claudio Ranieri lakini umethibitishwa na matokeo yao.

    Mabigwa hao watetezi wa klabu bigwa ulaya, hawajapoteza mechi yoyote tangu Ranieri, 65, alipopigwa kalamu mwezi Februari.

    Pia waliweza kufika robo fainali ya ligi ya Champions baada ya kupata ushindi dhidi ya Sevilla.

    Ranieri aliwaongoza Leicester, kwa ushindi uliowashangaza wengi kwa kulinyakua taji ya Premia mwaka 2016, lakini The Foxes walikuwa alama moja juu ya hatua ya muondoano na walikuwa wamepoteza michezo mitano ya ligi kabla ya kufukuzwa kwake.

    Leicester haikufunga goli lolote mwaka 2017, lakini wakiwa chini ya uongozi wa Craig Shakespeare ambaye anaiongoza timu hiyo hadi mwisho wa msimu huu, wamefunga magoli saba katika mechi tatu walizoshiriki.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako