• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kenya:Wataalamu wa kiuchumi wapongeza kupunguzwa kwa mishahara ya viongozi wa serikali.

    (GMT+08:00) 2017-03-17 20:15:02

    Siku moja tu baada ya rais Uhuru Kenyatta wa Kenya kupendekeza kupunguzwa mishahara ya viongozi wa serikali ya Kenya wakiwemo wabunge na magavana ,wataalamu wa kiuchumi wanasema hatua hiyo ni sahihi na itaboresha ushuru wa Kenya.

    Utafiti unaonyesha nusu ya ushuru wa wakenya unatumika na watu asilimia 2 ya wakenya wote ambao ni viongozi.

    Akitoa hotuba yake ya mwisho kwa taifa bungeni kabla ya uchaguzi, rais alisema kuwa gharama ya mishahara ya serikali kwa sasa ni shilingi bilioni 627 inayowakilisha asilimia 50 ya mapato yote ya nchi ambayo hulipwa mishahara kwa watumishi wa serikali ambao ni asilimia 2 pekee ya wafanyakazi humu nchini.

    Alisema hali hiyo isipochunguzwa maendeleo ya nchi hii yatakwama.

    Rais alitoa changamoto kwa viongozi waliochaguliwa kujizatiti kuwahudumia wakenya na sio kujinufaisha wao wenyewe.

    Aliwataka viongozi katika viwango vya kaunti na kitaifa kuunga mkono tume ya kuwianisha mishahara na marupurupu inapojiandaa kupunguza mishahara hiyo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako