• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais Xi Jinping wa China afanya mazungumzo na rais Paul Kagame wa Rwanda

    (GMT+08:00) 2017-03-18 18:30:37

    Rais Xi Jinping wa China jana alifanya mazungumzo na rais Paul Kagame wa Rwanda kwenye Jumba la mikutano ya umma. Marais hao wawili walikubaliana kuhimiza kutekeleza makubaliano yaliyofikiwa kwenye mkutano wa kilele wa baraza la ushirikiano kati ya China na Afrika huko Johannesburg, kutafuta njia mpya wa kufanya ushirikiano, kuzidisha ushirikiano wa kunufaishana na kuinua kiwango cha ushirikiano wa kimkakati kati ya nchi hizo mbili.

    Rais Kagame alisema kuwa, Rwanda inaheshimu uhusiano wa kirafiki na ushirikiano kati yake na China, ilishukuru mchango wa China kwa ukarabati na maendeleo ya Rwanda, na inakaribisha makampuni ya China kuongeza uwekeaji katika sekta za kilimo, madini, utalii na ujenzi wa miundo mbinu.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako