• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais Xi Jinping akutana na waziri wa mambo ya nje wa Marekani

    (GMT+08:00) 2017-03-19 15:51:54

    Rais Xi Jinping wa China leo hapa Beijing amekutana na waziri wa mambo ya nje wa Marekani Bw. Rex Tillerson ambaye yuko ziarani nchini China.

    Rais Xi Jinping amesisitiza kuwa uhusiano kati ya China na Marekani ni muhimu sana kwa nchi hizo mbili hata dunia. Maslahi ya pamoja kati ya China na Marekani ni kubwa zaidi kuliko mgongano kati yao, na ushirikiano ni njia sahihi ya pekee kwao.

    Bw. Tillerson amewasilisha salamu ya rais Donald Trump kwa rais Xi Jinping, akisema rais Trump anatilia maanani sana mawasiliano ya simu kati yake na rais Xi Jinping, pia anatarajia kukutana na rais Xi mapema, na kufanya ziara nchini China, ili kuthibitisha mwelekeo wa maendeleo ya uhusiano kati ya nchi hizo mbili katika miaka 50 ijayo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako