• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • IOC yailegezea masharti Kenya

    (GMT+08:00) 2017-03-20 09:29:49
    Kamati ya Kimataifa ya Olimpiki (IOC) imetangaza kuwa haitachukulia Kenya adhabu zaidi wakati huu kuhusu marekebisho ya katiba ya Kamati ya Olimpiki ya Kenya (NOC-K).

    Hata hivyo, Shirika la habari la Citizen limesema IOC itaendelea kuinyima NOC-K usaidizi wa kifedha kama ilivyotangaza juma lililopita kupitia barua iliyotiwa sahihi na Naibu wa Mkurugenzi Mkuu, Pere Miro na kuandikiwa rais wa NOC-K, Dkt Kipchoge Keino.

    NOC-K inatarajiwa kuchagua maafisa wapya baada ya katiba hiyo kutipishwa. Kenya ilikuwa inakabiliwa na tishio la kupigwa marufuku na IOC kwa sababu maafisa wa NOC-K walikuwa wamekataa kurekebisha katiba.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako