• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Shughuli za kuwachagua madaktari bora waliotoa msaada wa matibabu katika nchi za nje kuzinduliwa mwezi Aprili

    (GMT+08:00) 2017-03-20 18:16:23

    Shirikisho la Urafiki wa Watu wa China na nchi za nje, kamati ya afya na uzazi wa mpango ya China, pamoja na idara ya ugavi ya Jeshi la Ukombozi la Umma la China, zimesema mchakato wa kuwatafuta madaktari bora waliotoa msaada wa matibabu katika nchi za nje utazinduliwa mwezi ujao.

    Katika mchakato huo, madaktari kumi watakaochaguliwa watapewa tuzo ya "madaktari bora" kwenye hafla itakayofanyika mwezi Agosti hapa Beijing.

    Naibu mkurugenzi wa Idara ya ushirikiano wa kimataifa ya Kamati ya afya na uzazi wa mpango ya China Bw. Feng Yong amesema,

    "Tangu mwaka 1963, China ilianza kupeleka madaktari katika nchi zinazoendelea, hii imekuwa njia muhimu ya China kutoa msaada katika nchi za nje, hali ambayo imeonesha umuhimu mkubwa katika kuimarisha uhusiano kati ya China na nchi nyingine zinazoendelea na kuhakikisha afya ya watu wa nchi hizo."

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako